TMA YATANGAZA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA


Na Mwandishi Wetu,

Mamlaka ya hali ya hali ya hewa nchini TMA, imetangaza kuwa msimu wa mvua za masika zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani huku maeneo mengine yakipata mvua za wastani hadi juu ya wastani

Akizungumza wakati wa mkutano na vyombo vya habari katika Ofisi za TMA-Dar es Salaam, Ubungo Plaza, tarehe 22/02/2023, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a amesema maeneo yatakayopata mvua za juu ya wastani ni pamoja na Dar es salaam mkoa wa Pwani,Unguja na Morogoro kaskazini.

Aidha, ameongezea kuwa Ongezeko la mvua linatarajiwa katika kipindi cha mwezi Mei 2023, hususan katika maeneo ya pwani ya kaskazini

Awali Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka TMA, Rose Senyangwa amesema mifumo ya hali ya hewa joto la bahari la wastani hadi juu kidogo ya wastani linatarajiwa katika eneo la kati la bahari ya pasifiki, joto la wastani linatarajiwa katika eneo kubwa la kitropiki la bahari ya Hindi huku joto la juu ya wastani likitarajiwa katika eneo la Mashariki mwa Bahari ya Atlantiki hali hiyo itadhoofishamifumo inayosababisha mvua.

Hatahivyo kwa mwaka 2022 utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ulifanikiwa kwa kiwango cha asilimia 94 hivyo wataendelea kutoa mrejesho wa mwelekeo wa mvua nchini kadri inavyohitajika na kuwashauri wadau kuwasiliana nao ili kupata taarifa mahsusi za utabiri wa msimu ili kukidhi mahitaja maalum katika sekta zao.
Previous Post Next Post