TMA YASISITIZA UMUHIMU WA KUTOA TAARIFA KWA USAHIHI NA KWA WAKATI


Na Mwandishi Wetu

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Ladislausi Changa katika warsha ya wanahabari kuhusu utabiri wa mvua za msimu wa masika (Machi hadi Mei 2023) iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Dkt. Changa amesema utabiri huo wa mvua za masika utakaotolewa utakuwa wa 22 toka kuanza kwa utaratibu wa kutoa taarifa hizo za hali ya hewa hapa nchini.

Aidha amesema wana mkakati wa kuhakikisha kuwa utabiri wa hali ya hewa uwe unatolewa kwa maeneo madogo madogo ili kuwezesha jamii kupata taarifa za hali ya hewa katika maeneo yao.

Sambamba na hayo amewapongeza waandishi wa habari kwa jitihada zao za kutoa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa wakati na uhakika pamoja na kuielimisha jamii na kuhusu taarifa za tahadhari za hali ya hewa na athari zake.

Dkt. Chang’a amesemaKuongezeka kwa muamko na taarifa za hali ya hewa ni muhimu kutokana na changamoto za hali ya hewa duniani ambapo kwa sasa joto duniani linaongezeka ambapo kila mwaka joto duniani huongezeka ambapo inatarajiwa kufikia nyuzi joto 1.5 ifikapo mwaka 2030 kama jitihada za kupunguza ongezeko hilo la joto hazitachukuliwa.

Hata hivyo amesema kuna haja ya hatua stahiki kuchukuliwa kuelimisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira na kuzingatia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini.

Mvua za msimu wa masika ni mahususi kwa mikoa ya kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa na Pwani ambayo ni muhimu kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo.
Previous Post Next Post