KATIBU MKUU DKT. YONAZI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA TAASISI YA TECDEN

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania ECD Network (TECDEN) Bi. Mwajuma Kibwana (kushoto) pamoja na Bi. Merina Maneno Afisa Utawala wa Taasisi ya TECDEN walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma tarehe 07 Mei, 2024.



Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania ECD Network (TECDEN) Bi. Mwajuma Kibwana (kushoto) walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.Kulia ni Bi. Merina Maneno Afisa Utawala wa Taasisi ya TECDEN.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akisalimiana na Bi. Merina Maneno Afisa Utawala wa Taasisi ya TECDEN walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma na kufanya mazungumzo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Tanzania ECD Network (TECDEN) Ofisini kwake Jijini Dodoma tarehe 07 Mei, 2024.Kushoto ni Mkurudenzi Mtendaji wa TECDEN Bi.Mwajuma Kibwana na wa kwanza kulia ni Bi. Merina Maneno.



(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)



Na Mwandishi wetu.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Taasisi ya Tanzania ECD Network (TECDEN) Jijini Dodoma.

Dkt. Yonazi amekutana na uongozi huo Mei 7, 2024 ambapo walijadili kuhusu kazi za Taasisi hiyo ikiwemo ya uratibu wa Mashirika na Wadau wasio wa Kiserikali katika masuala mazima ya malezi, makuzi ya awali ya watoto wadogo kuanzia umri 0 hadi miaka 8.

Katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa Serikali  itaendelea kushirikiana na Wadau ikiwemo Taasisi hiyo ili kuendelea kuleta matokeo yenye tija kwa Taifa.
=MWISHO=



Previous Post Next Post