RAIS SAMIA ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KIZIMKAZI ZANZIBAR


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Agosti 24,2024 ametembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii na kujionea vivutio mbalimbali vya wanyamapori kwenye maonesho ya Tisa ya Tamasha maarufu la Kizimkazi Kusini Unguja visiwani Zanzibar.

Akiwa katika banda hilo, huku akiongozwa na mwenyeji wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amejionea wanyamapori mbalimbali kama Simba, Pundamilia, Chui, Fisi n.k.

Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro zimeshiriki Maonesho hayo.
Previous Post Next Post