NIT YASAINI MKATABA WA UJENZI WA KITUO CHA UMAHIRI NA MAFUNZO YA TAALUMA YA USAFIRI WA ANGA


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam

Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Caroline Nombo amekiagiza Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT kutafakari kuangalia mahitaji ya nchi katika sekta mbalimbali kwa kutoa taaluma za masuala ya anga ili kuzalisha wataalamu wazawa katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi.

Prof. Nombo ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini ujenzi wa kituo cha umahiri mafunzo ya taaluma ya usafiri wa anga na oparesheni za usafirishaji ambayo ni majengo matano katika chuo hicho kwa ufadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa ESTREP ujenzi utakaogharimu Shilingi bilioni 21.


Hata hivyo Profesa Nombo amesema malengo ya serikali ni kuhakikisha vyuo vya kimkakati ikiwemo chuo hicho cha NIT vinatoa mafunzo yanayoakisi mahitaji ya nchi na kutatua changamoto zinazokabili nchi yetu katika sekta mbalimbali.

"Kwa wakandarasi ninawaomba mfanye kazi kwa bidii na uweledi ili kuhakikisha kuwa mradi unakamilika kwa muda uliopagwa yaani miezi 12."amesem Prof Nombo


Aidha amewataka wakandarasi hao kujenga majengo bora kulingana na thamani yake pia kukabidhi majengo hayo kwa muda wa makubaliano ya kwenye mkataba. 

Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Prof. Zacharia Mganilwa amesema tayari baadhi ya vifaa vya kufundishia taaluma umahiri wa mafunzo ya usafiri wa anga vimeshafika hivyo ujenzi wa majengo hayo ni chachu katika mendeleo ya sekta ya elimu nchini.

Amesema chuo hicho kimeanzisha kituo cha umahri katika taaluma ya anga na masuala yote ya usafirishaji ambapo tayari NIT imefikia asilimia 75 ya utekelezaji. 


Ujenzi wa majengo hayo matano yanayotarajiwa ni pamoja na majengo ya mafunzo ya umahiri wa taaluma ya usafiri wa anga, wahudumu wa ndege, karakana ya kisasa ya miundombinu ya anga pamoja na mabweni ya wanafunzi.
Previous Post Next Post