RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MWINGINE, MCHECHU AWA MSAJILI WA HAZINA


Na Mwandishi Wetu

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Nehemia Kyando Mchechu, kuwa Msajili wa Hazina. 

Kabla ya uteuzi huo Bw. Mchechu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).  Bw. Mchechu anachukua nafasi ya Bw. Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.

 Amemteua Bw.Hamad Abdallah, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). 

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Abdallah alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Gimcoafrica Limited na anachukua nafasi ya Bw. Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina. 



Previous Post Next Post