VETA KUSHIRIKIANA NA JKT KATIKA KUWAWEZESHA VIJANA KUPATA MAFUNZO YA UFUNDI STADI


Na Paul Kayanda, Mbeya
Augost 3,2023

MENEJA wa Mamlaka ya elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Sitta Peter amesema kuwa watanzingatia mawazo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa kuhusu vijana wanaokwenda kujiunga na mafunzo ya JKT ambao licha ya kujifunza ukakamavu wanajifunza pia masuala ya ufundi wa aina mbalimbali kama masuala ya uzalishaji na kuongeza kuwa Waziri alizungumza kuwa Veta inaweza ikaingia makubaliano na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa JKT kuwasaidia hawa vijana pindi wanapotoka kwenye mafunzo hayo wawe na shughuli zinazotamburika.


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa JKT Innocent Bashungwa jana alitembelea banda Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya ufundi stadi ( VETA ) ambako alitoa maelekezo pamoja na ushauri mbalimbali juu ya vijana wanaojiunga na JKT.


Meneja huyo wa mamlaka ya elimu na mafunzo stadi alisema kuwa kama makubaliano hayo yatafikiwa vijana watatumia muda wao wa mafunzo hayo miezi kadhaa watajifunza ukakamavu na uzalendo lakini miezi mingine watajifunza ufundi stadi katika maeneo mbalimbali na wakatunukiwa vyeti wakirudi mitaani watatumia ujuzi walioupata kupata ajira.


Kauli mbiu kwa mwaka huu, ''Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu na chakula''



Previous Post Next Post