NHC yajipanga kuishawishi Serikali kuruhusu Diaspora kuwekeza nchini



Na Iddy Ally 

SEKTA ya Nyumba nchini iweze kupata ustawi na kukua zaidi, Shirika la Nyumba la Taifa NHC limejipanga kuendelea kuishawishi serikali kuwa nyumba ni kipaumbele cha Taifa ambapo hadi sasa juhudi zinafanyika kuwaruhusu Diaspora kununua nyumba na kuwekeza katika ardhi ya Tanzania.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi mkuu wa NHC Hamad Abdallah katika mkutano wa wahariri na waandishi wa vyombo vya habari nchini kuelezea kazi zinazofanywa na shirika hilo jijini Dar Es Salam.

Amesema kasi ya ukuuaji wa uchumi inazidi kuongezeka ambapo kwa sasa shirika lina nyumba za bei nafuu kila mkoa kwa ajili ya Watanzania wenye uhitaji wa nyumba za makazi.

Akizungumzia sera ya Ubia kati ya NHIC na sekta binafsi Hamad amesema kwa sasa imefungua milango ya uwekezaji kwenye sekta ya nyumba na kuendelea kuvutia wawekezaji nchini kupitia sekta binafsi ambayo ni injini ya kujenga uchumi imara.

Aidha akizungumzia mpango wa matengenezo ya nyumba za Shirika amesema sambamba na ukusanyaji wa kodi shirika limetumia Bilion 6 kukarabati nyumba 847 maeneo mbalimbali na bado ukarabati unaendelea pamoja na kuanzishwa kwa mradi mpya wa ujenzi wa nyumba za makazi ujulikanao kama Samia Housing Scheme utakaohusisha ujenzi wa nyumba 5000.

Sambamba na hayo, NHC imetangaza kuja na mpango wa kuwatangaza wadaiwa sugu kwenye vyombo vya habari na kuwataka wateja wao kuzingatia na kufata masharti na taratibu za upangaji wa nyumba za shirika hilo.

Akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa jukwaa la wahariri TEF Deodatus Balile, Liliani Tumbuka amesema hii ni nafasi ya kipekee itakayosaidia kuchochea maendeleo ya nchi kwa kutoa wigo kwa wananchi kutambua shughuli mbalimbali za mashirika ya Umma na kutoa wito kwa mashirika mengine kuendelea kufanya kazi kwa karibu na wahariri na waandishi wa habari kuhabarisha Umma kazi za mashirika hayo.

 Shirika la Nyumba La Taifa NHC lilianzishwa rasmi mwaka 1962 mwaka mmoja baada ya Tanzania kupata Uhuru likiwa ni shirika la kwanza la serikali kuanzishwa chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo thamani ya mali za shirika hadi kufikia Juni 31,2022 ni trilioni 5.04 na kuzalisha faida ya shilingi bilioni 60.7 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Previous Post Next Post