MUSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI KUTUA BUNGENI LEO


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema muswada wa mabadiliko ya sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 utatua bungeni leo Februari 10, 2022.


Nape amebainisha hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mabadiliko ya ratiba za Bunge na sasa muswada huo uliokuwa uwasilishwe kwenye Bunge la Aprili, sasa utasomwa kwa mara ya kwanza leo.

Juzi, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alitoa taarifa kwamba muswada huo hautaweza kusomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa Bunge unaokwisha kesho, badala yake utasomwa katika mkutano ujao wa Bunge.


Wadau wa sekta ya habari wamekuwa wakishinikiza sheria hiyo ifanyiwe marekebisho makubwa kwa sababu ina vifungu vingi ambavyo vinakwamisha uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini.

Previous Post Next Post