AIRTEL YATANGAZA KUTOA FIDIA YA SHILINGI BIL. 1.6 KWA WATEJA WAKE


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza kutoa faida ya Tzs 1.6 bilioni kwa wateja na mawakala ambao wamekuwa wakitumia huduma ya Airtel Money kwa kipindi cha Julai mpka Septemba 2022.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati anatangaza kuanza kutoa Gawio la faida la Airtel Money, Mkuu wa kitengo cha Huduma za Airtel Money Daudi Ndovu amesema gawio hilo litatolewa kwa wateja na mawakala wote ambao walikuwa wakitumia huduma za airtel money kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2022 kote nchini kuanza leo.

Aidha Ndovu amesema kuwa Airtel imedhamiria kuendelea kuboresha na kuleta huduma za Airtel Money karibu na wateja na kufikia Watanzania ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki hasa maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake Meneja Uhusiao wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando amesema Airtel inaendelea na dhamira yake ya kuwekeza kwenye kupanua wigo wa mtandao wa airtel Money ili kuendelea kutoa huduma zilizo bora zaidi.

Faida ya Gawio la Airtel hutolewa kwa wateja,wadau na mawakala wa Airtel Money kwa kila robo ya mwaka kulingana na kiasi kilichopo kwenye akaunti zao za Airtel Money.
Previous Post Next Post