MAWAKALA WA BENKI YA NBC KUPATIWA VYETI VYA BIMA


Na Mwandishi Wetu

Benki ya NBC kwa kushirikiana na kampuni ya Bima Jubilee imewatunuku Vyeti mawakalawa Benki ya Biashara(NBC) waliofanya mtihani na kufaulu katika mafunzo ya Bima kwa mawakala wote nchini Tanzania wa Benki NBC yalioanza mwezi Disemba 2022 katika chuo cha Afrika college of Insurance.

Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja Mkuu Msaidizi wa Jubilee Allianz, Abdul Rauf amesema wametoa vyeti kwa asilimia 90 kati ya mawakala 100 ywaliofaulu mitihani ikiwa ni wiki chache zilizopita baada ya kupatiwa mafunzo ya uuzaji Bima kukamilika.


"Kampuni ya Bima ya Jubilee Allianz kushirikiana na Benki ya NBC, ilichagua mawakala wa huduma za kifedha, kuwadhamini na Kuwapeleka mafunzo ya muda mfupi katika chuocha Africa College of Insurance and Social Protection kwaajili ya kupatiwa elimu ya Bima, Leo Tar 9 Februari 2023, Mawakala hao wamepatiwa vyeti vyao sasa Rasmi kuruhusiwa kufanya biashara ya Bima,"amesema Abdul.

Ameongeza kuwa Benkinya NBC kwa Kushirikiana na kampuni ya Bima ya jubile Allianz wataendelea kutoa elimu ya BIMA kwa mawakala na wanatarajia kifikia mwezi sita wawe wametoa mafunzo kwa mawakala wasiopungua 6000 huku akisema lengo kuu ni kuongeza urahisi wa upatikaji wa BIMA nchia na kulikuza soko la BIMA.

Aida ametoa wito kwa wahitimu kutoa huduma bora kwa wateja na kuwapa. elimu ili kuhakikisha kuwa wanasogeza zaidi huduma ya bima kws wateja wao.



Kwa upande Wake Mkuu wa kitengo cha Bima NBC, Benjamini Mkaka amesema mpango walio nao ni kufanya kazi kwa ukaribu na wakala hao na kuendelea kupeana elimu, kupitia kila katikaa maeneo yao kazi na kuelezea pale amabapo kuna changamoto na kusaidia kutatua kwa haraka.

"Ninyi mmfekuwa wanafuaka wa kwanza na mtafungua mlimgano kwa mawakala wengine, na ifikapo mwezi wa sita tunatarijia kuwafikia mawakala 6000,"amesema Benjamini.
Previous Post Next Post