IFAD NA MAWAZIRI WA TANZANIA WAKUTANA ITALIA KUJADILI MAENDELEO YA UVUVI

Rais wa Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo duniani Mhe. Alvaro Lario wa IFAD akiwa na Viongozi waandamizi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Waziri wa mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki, Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe Mahmoud Thabiti Kombo na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia






Na Mwandishi Wetu,
Rome,Italia.


Mkutano wa Mfuko wa Maendeleo wa Kilimo na Uvuvi Duniani (IFAD) umeanza mapema jana Februari 13, 2023 ukihudhuriwa na Rais wa Mfuko huo, Alvaro Lario pamoja na Mawaziri wa Uvuvi kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ambapo wamejadili mambo mbalimbali juu ya sekta ya uvuvi.

Katika mkutano huo, viongozi hao waandamizi ni pamoja na Mawaziri wawili wa Uvuvi na Makatibu Wakuu wawili, wakiongozwa na Waziri wa Uvuvi Mashimba Ndaki sambamba na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Balozi Mahmmoud Thabiti Kombo ambaye pia ni Mwakilishi wa kudumu wa mfuko huo wa IFAD akiwakilisha Tanzania,

Miradi inayojadiliwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa meli za uvuvi, ujenzi wa masoko, majokofu ya baridi ya kuhifadhi samaki na mazao ya baharini ikiwemo mwani.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ambao unatarajiwa kufikia mwisho Februati 16,2023, ni moja na timu ya maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia wakiongozwa na Mwambata wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Misitu, Jaquiline Mhando.
Previous Post Next Post