JWK YAVUTIWA NA DAWATI LA UWEZESHAJI BIASHARA LA FORODHA





Na Mwandishi Wetu……

Uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK) umefanya ziara ya kutembelea dawati maalum la uwezeshaji biashara Kariakoo katika Idara ya Forodha na Ushuru ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kupongeza namna huduma zinavyotolewa katika kurahisisha biashara.


Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo Bw. Sevelin Mushi amesema dawati hilo limekuwa kiungo baina yao na TRA upande wa Forodha na linasaidia kurahisisha biashara kwa kuondosha mizigo kwa haraka Zaidi tofauti na awali.


Amesema dawati hilo ni mkombozi kwa wafanyabiashara wa Kariakoo kwani linawasaidia kufanya ufuatiliaji wa mizigo yao pindi wanapoagiza na kutoa wito kwa wafanyabiashara wa Kariakoo kulitumia dawati hilo kurahisisha biashara zao.


Bw. Apolinary Kiwango ni mfanyabiashara anayeingiza mizigo kutoka nchini China ambaye amesema dawati hilo linasaidia kuleta usawa na ushindani uliosawa sokoni kwa kuhakikisha kila mtu analipa kiwango cha kodi anachostahili.



Bw. Renatus Mlelwa ni Katibu wa JWK ambaye amesema kupitia dawati hilo wanaweza kupata taarifa sahihi za mizigo yao pindi wanapoagiza na kueleza kuwa kusomana kwa taarifa za Forodha na Kodi za ndani kutakuwa na manufaa makubwa kwa. 





Kwa upande wake Meneja wa Forodha Bw. Anangisye Mtafya amesema dawati hilo ni kiunganishi baina ya Forodha na wafanyabiashara wa Kariakoo na limeanzishwa mahususi ili kuwezesha biashara na kuwataka kulitumia dawati hilo kupata huduma na kutatua changamoto zinazowakabili.

= = = = = = =

Previous Post Next Post