WAZIRI GWAJIMA: WANAWAKE CHANGAMKIENI FURSA ZA KIUCHUMI IKIWEMO KUCHUKUA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU


Na Lilian Ekonga 

Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima amewaasa wanawake Nchini kuchangamkia fursa hasa za kiuchumi ikiwemo kuchukua mikopo yenye riba nafuu ili waweze kujiinua kimaendeleo na kiuchumi. 

Hayo ameyasema katika hafla ya uzinduzi wa Akaunti ya Fanikisha Mwanamke Hodari kutoka azania banki iliyofanyika jijini dar es salaam ambapo ameipongeza benki ya azania kwa kuja na wazo la kufungua akaunti kwaajili ya wanawake yenye liba nafuu ya asilimia moja. 

"Dizaini ya akaunti mwanamke hodari fanikisha kutoka azania benki naona inagusa makundi maalumu moja kwa moja hata mfanyabishara mdogo anaweza kuchukua mkopo na kurudisha liba nyenye nafuu kabisa" amesema Gwajima. 

Amesema benki ya azania kwa kuwa miuongoni mwa benki zinazotoa kipaumbele kwa wanawake kwa kuja ya akaunti ya kumkombea wanamke kiuchumi na kuwasihi waendelee kusongesha kusong gurudumu hilo ilibenki yao iweke kukua

Waziri ameongeza kuwa kaunti hiyo itaweza kusaidia kinamama katika familia katika kuwasaidia kibaba hasa katika majukumu ya nyumbani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Azania banki, Rhimo Nyansho amesema lengo la kuanzisha akaunti ya fanaikisha mwanamke hodari ni 
kuwayasapoti makundi yote na kuhakikisha wanaleta matokeo ambayo yanawesa kusababisha mtu ajikwamue kutoka sehemu moja kwenda nyingine.


"Kuna makundi ambayo yanaweza kulete matokeo mazuri hasa katika kundi la kinamama na kundi la vijana.tunaamini kwa kinamama wakikopa wanalipa"amesema Nyansho.

Amesema licha ya kupata faida kupitia akaunti ya fanikisha kiu yao kubwa kama benki ni kuleta matokeo chanya katika kile kitu wanachokifanya. 

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Azania banki Esther Mangenya amsema kila mwanake ili afanikiwe lazima awe hodari na ndomna wamekuja na jina la Hodari na 
Akaunti itakuwa na unafuu ukitofautisha na akounti zaingine pia ni rahisi na haina makato na ina lipa nafuu.
Previous Post Next Post