SERIKALI IMEWASIHI WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI ZINAZOTOKANA NA USHIRIKIANO KATI NA TANZANIA NA MAREKANI


Na Mwandishi Wetu,

Serikali imewasihi watanzania kuendelea kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotokana na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali ikiwemo Marekani na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuliletea maendeleo taifa. 

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) alipozungumza na waandishi wa Habari kuelezea mafanikio ya ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris aliyoifanya nchini tarehe 29 – 31 Machi, 2023.

Dkt. Tax amesema ziara ya Mhe.Kamala Harris, nchini imekuwa na mafanikio makubwa katika kuimarisha na kufungua maeneo mapya ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani na kuitangaza Tanzania duniani. 

Amesema kupitia ziara hiyo, Serikali ya Marekani ilitoa ahadi mbalimbali kwa Serikali ya Tanzania na Mikataba na Hati za Makubaliano kusainiwa ambapo Serikali ya Marekani itajenga kiwanda kikubwa nchini kitakachokuwa cha pekee barani Afrika. Kiwanda hicho cha kuchakata madini ya Nikel yanayotumika kutengenezea betri za gari za umeme kwa ajili ya soko la Marekani na duniani ifikapo mwaka 2026.  


"Serikali ya Marekani kupitia Mpango wa Rais wa kupambana na Malaria (Presidential Malaria Initiative) kutenga kiasi cha Dola za Marekani milioni 39 kwa mwaka 2024. Mradi huo unalenga kupambana na malaria, ikiwa ni pamoja na kusambaza vyandarua, dawa za malaria, vifaa vya uchunguzi wa haraka wa malaria, na dawa za kuzuia malaria kwa wajawazito, ambapo Tanzania itaendelea kunufaika" amesema.
Previous Post Next Post