ROYAL TOUR YA FUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI MIRERANI



Na Mwandishi Wetu, Manyara 

MKURUGENZI wa Kampuni ya Ngabomoa Hotel,Gaspal Ngabomoa Swai ambaye ni mmiliki wa Ngabomoa Tembo raha Hotel na Montel lodge iliyopo katika mji mdogo wa Mirerani wilaya Simanjro Mkoani Manyara amaesema anawakaribisha wadau na wafanyabishara mbalimbali ambao ni wateja wao hususani walioko ndani ya Mamlaka ya mji mdogo  Mirerani na Tanzania kwa ujumla na nje ya nchi ili waje kupata huduma nzuri na yenye viwango vya kimataifa.


Pia amesema kuwa kuelekea sikukuu  za Pasaka na Id –El Fitir wanatarajia kufanya uzinduzi mkubwa wa Kilabu yao ambayo ni kilabu ya kisasa nakwamba ameamua kufanya uwekezaji huo mkubwa kutokana na aina ya maisha ambayo alikuwa ameyaishi huko nyuma na ndio maana ameweza kufanya uwekezaji mkubwa na kwakuanzia amewekeza katika ujenzi wa hotel kubwa ya kisasa ambapo ndani yake ndio kuna kulabu.


Mkurugenzi Ngabomoa ameyasema haya Aprili 6 mwaka huu wakati akazingumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambao pia walifika hotelini hapo kwa lengo la kujionea uwekezaji huo mkubwa iliofanywa na Mtanzania mzawa,ambapo pamoja na mambo mengine ameweza kutoa ajira nyingi kwa vijana wakitanzania ambao wanaendesha maisha yao kupitia uwekezaji wake.


“Kwakweli  katika maisha yangu nilipitia changamoto kubwa sana na ndio maana nikaamua kufanya uwekezaji huu hususani hapa Mirerani na kimsingi niliamua kujiajiri mimi mwenyewe  na pia niweze kuajiri watanzani wezangu na nimetoa fursa ya ajira kwa watanzania wezangu na kadri inavyokwenda nitaendelea kuajiri watanzania zaidi na hapa namshukuru sana mhRais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa moyo wake wa upendo ambao ameweza kuleta Royal tour ambayo inatoa fursa ya kupata wageni mbalimbali ambao hawa wakipita wananunua vitu mbalimbali na wengine kupata maradhi kwenye maeneo kama haya kwakweli Rais Samia ameupiga mwingi.’’amesema Mkurugenzi Ngabomoa.


Ameongeza kuwa katika kipindi chake cha miaka miwili ya rais Samia ameweza kurudisha hali ya mshikamano na amani na amekuwa akitetea hata wafanyabiashara kweli wataendelea kumuunga mkono ili mama aendelee kufanya vizuri katika uongozi wake na kuhusu uwekezaji yeye binafsi ameamua kuwekeza mirerani japokuwa changamoto ni nyingi lakini amemua kutafuta faida ya kinyonga ya kidogo kidogo.


Amefafanua kuwa amependa kufanya hivi kwasababu alipofika eneo hilo aliona awekezaji tu katika eneo hilo kwani hakuna mahala pengine pa kuwekeza kikubwa serikali iliendelee kusaidia kwa kuweka miundimbinu mizuri ili kuleta muungano mzuri kama wanavyofanya pale kwenye mgodi wa Tanzania basi wafanye na maeneo mengine ili wageni waweze kuja kwa wingi na pindi wanapokuja wageni na wao ndio wanapata kidogo kidogo faida.



Amesema kuwa mirerani panahitaji kujengwa kwasababu ukiondoa uwepo wa mgodi lakini panamakazi ya watu ya kudumu lakini hakuna vyuo hivyo serikali waendelee kuunga mkono ili wao waendelee kuwekeza  na kikubwa zaidi wakazi wa eneo hilo hasa wafanyabishara warudi kuwekeza kwenye eneo hilo ili kupafanya kukua kama ilivyo kwenye maeneo mengine.

“Nawaalika watanzania wote wafanyabishara ,wadau ,watalii kuja katika hotel yake ya Ngabomoa ili kupata huduma zote wanazohitaji kwani pana kumbi za kisasa , maegesho makubwa ya magari ,chakula, vinywaji vyote vipo ,malazi kwa maana sehemu ya kulala, na kuelekea sikuku patakuwa na uzinduzi mkubwa wa kilabu lengo watu wakija wafurahie huduma.’’amesema 


Na Kwaupande wake Meneja wa Hotel hiyo Dismas Deus Kagandiga  na msaidizi wake Halima Hamza wamesema kuwa Hotel hiyo Ngabomoa inapatikana katika mtaa wa Songambele uliopo katika mji huo mdogo wa Mirerani na kuhusu huduma amesema wanatoa huduma mbalimbali kama alivyotangulia kusema mkurugenzi wao  hivyo anawakaribisha watanzania wote kumuunga mkono Ngabomoa ukizingatia eneo hilo kwa muda mrefu lilikosa maeneo ya watu kupata furaha hivyo wao wanakwenda kutengeneza fursa ya wakazi wa mirerani na maoneo mengine ya jirani 


Amesema kuwa Aprili 8 mwaka huu wanatarajia kuzindua jengo na matarajio yao nikupokea wageni wa kutoka maeneo mbalimbali na katika uzinduzi huo watakuwa na wasanii wengi akiwepo Kusah kutoka jijini Dar es Salaam na kimsingi eneo hilo halikuwahi kupata wageni wengi hivyo kwa ukubwa wa eneo lao na namna walivyojipanga kila kitu kitakuwa sawa na watu watapata burudani nzuri sana
Halima ameongeza kuwa katika hoteli hiyo inakwenda kuzindua ukumbi wa kipekee na wa kwanza kwa mji wa mirerani na wamejipanga kwa kila kitu kwani kuna  usalama wa hali ya juu kuna kamera na kila kitu ,wahudumu ni walembo watakuwa wamevalia sare  maalumu  ambazo zitawatambulisha kama wao ni wahudumu hivyo anawakaribisha sana  sana watanzania wote.
Previous Post Next Post