ACT WAZALENDO YAISHAURI SERIKALI KUWEKEZA KWA WAKULIMA WADOGO

Na Mwandishi Wetu,

 Chama cha ACT Wazalendo kimeiomba serikali kuhakikisha mazingira bora yanawekwa kwa ajili ya wakulima wadogo nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku katika mbolea na kusimamia usambazaji wake, na kuhakikisha usalama wa ardhi kwa wakulima hao. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Dorothy Semu, amesema serikali inapaswa kununua na kuhifadhi chakula cha kutosha angalau kwa miezi mitatu ili kujilinda dhidi ya upungufu wa chakula.

"Kwa kuwa uzalishaji katika maeneo mengi nchini unaweza kuwa duni mwaka huu, hatua hii itawezekana kwa serikali kujenga uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa kutenga bajeti ya kutosha ya kununua chakula, ikiwa ni pamoja na tani milioni 1.5 za mahindi, tani laki 5 za mpunga, na maharagwe tani milioni 1," amesema Dorothy.

Aidha, ameishauri serikali kuwezesha bodi ya mazao mchanganyiko kwa kununua na kusambaza chakula kwenye maeneo yanayoonyesha uhaba au upungufu wa chakula. Pia, ACT Wazalendo wameziomba serikali kuja na sera mpya ya fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo ya uwekezaji, ambapo kila ardhi iliyopishwa itumike kama mtaji katika mradi na kuzipa serikali za mitaa umiliki katika miradi husika.

"Wananchi wajengewe makazi mbadala katika maeneo yaliyopimwa na yenye huduma zote za kijamii, na vilevile wapewe shughuli mbadala za kiuchumi kama vile ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, na kilimo," amesema.

Kwa upande mwingine, ameiomba Ofisi ya Waziri Mkuu ieleze lini muswada wa Sheria ya Vyama Vingi vya Siasa 2023 na Muswada wa Sheria ya Uchaguzi 2023 utafikishwa Bungeni ili kufanikisha mchakato wa katiba mpya.
Previous Post Next Post