RAIS DK. MWINYI: TUONGEZEE BIDII YA KUSOMA QUR'AAN NA TUWASAIDIE WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU


Na Mwandishi Wetu,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, ambaye amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Sami ina Suluhu Hassan, katika Mashindano makubwa ya Qur'aan ya Afrika, amesema uwepo wa mashindano hayo ni fursa ya kipekee kuitangaza Tanzania Kimataifa na kuiletea manufaa kwa kufuatiliwa kupitia mitandao ya kijamii na njia nyingine za mawasiliano.

Aliyasema hayo leo wakati akihutubia wananchi katika Mashindano makubwa ya Qur'aan ya Afrika mwaka 2023 yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo tarehe 09 Aprili, 2023, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al Hikma Foundation.

Rais Dk. Mwinyi amewahimiza waumini wa dini ya Kiislamu kuongeza bidii kusoma Qur'aan mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya mwezi kuisha ili kutekeleza ibada kwa usahihi.

Aidha, Dk. Mwinyi amewahimiza watu wenye uwezo kutoa sadaka kwa kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu kama yatima, wajane, walemavu, na wengineo hasa ndani ya mwezi huu wa Ramadhani.

Mashindano hayo makubwa ya Qur'aan ya Afrika mwaka 2023, ambayo yameshirikisha washiriki kutoka nchi ishirini za Afrika na washiriki watatu maalum kutoka Marekani, Uingereza na Saudia Arabia.

Pia, amewakabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza kutoka Misri kiasi cha shilingi 23,900,000 na medali ya dhahabu na laptop moja.

Mshindi wa pili kutoka Senegal amepokea shilingi 15,300,000 na medali ya fedha, Mshindi watatu kutoka Tanzania amepokea shilingi 10,280,000 na medali ya fedha.
Previous Post Next Post