Na Lilian Ekonga
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Songoro Mnyonge ameishauri jamii kutunza mazingira safi ya fukwe za Bahari ili ziweze kuwa chachu katika kukuza utalii nchini.
Mheshimiwa Mnyonge ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa akikabidhi kombe la Betika Sodo for Climate yenye lengo la kutunza mazingira ya ufukwe.
Aidha,Mnyonge amesema fukwe zikitunzwa vizuri zitaweza kuleta manufaa kwenye nchi ikiwemo sekta mbalimbali.
"Tumeona umuhimu wa kutunza fukwe hizi leo mchezo wa mpira wa soka la ufukweni hapa,mpira umechezwa hapa yote haya ni manufaa ya kutunza fukwe zetu"Amesema Mnyonge.
Kadhalika,Aidha, mheshimiwa Mnyonge ameishukuru BETIKA kwa kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa kauli mbiu isemayo "Shabikia Soka na siyo uharibifu wa Mazingira"
Naye Meneja wa Betika,Samwel Lawarence,amesema Sodo ni ligi ambayo imeleta Hamsha kuelekea mtoko wa kibingwa awamu ya 5 ambapo wanawake na wanaume wameshiriki.
"Tangu tumeanza kampeni ya mtoko wa kibingwa tumefanikiwa kuleta jumla washindi 400 kwa ndege kutoka mikoa yote nchini ambapo Msimu wa 4 washindi wa mtoko wa kibingwa walikuwa 50 saivi wameongezeka mpaka 100"Amesema Lawarence.
Hata hivyo,Lawarence amebainisha kuwa namna washindi walivyoshiriki Mtoko wa kibingwa ni kwakuweka mikeka mitano kwa siku yenye dau la jerojero mechi tatu na kuendelea, ambapo unaingia katika droo za kila wiki kushinda tiketi ya ndege na tiketi ya VIP A uwanjan katika mechi ya simba na Yanga.