Na Mwandishi Wetu
JUMLA ya walimu zaidi ya elfu sitini wamenufaika na mradi wa shule bora kwa kupewa elimu na mbinu za kufundishia ili kuweza kusaidia kukuza elimu nchini.
Hayo yamebainishwa leo jiji Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya elimu sayansi na Teknolia,Dkt Franklin Jasson Rwezimula,wakati wa mkutano na Wahariri wa Vyombo vya habari nchini.
Dkt Rwezimula amesema mradi huo wa miaka mitano umeanza mwaka 2021 unatarajia kumalizika 2027 utakuweza na jukumu la kuboresha mazingira ya elimu ikiwemo kuhakikisha shule moja inakuwa na mazingira yote ya ufundishaji.
"Mradi huu ambao unafadhiliwa na nchi ya uingeleza kupitia UKA ni wa mikoa tisa na katika mradi huu kwa kipindi kifupi umeweza kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya elfu sitini yote ni kukuza sekta ya elimu"amesema dkt Rwezemula.
Aidha,Dkt Rwezemula amesema lengo la serikali kuwa miradi hiyo ni kuhakikisha sekta ya elimu inaboreka.
"Kwa sasa kama mnavyojua serikali ipo kwenye kufanya mageuzi makubwa ya elimu nchini katika ngazi mbali mbali ,huu mradi ma shule bora nayo ni muendelezo wa mikakati wa kuboresha elimu"Amesema Dkt Rwezemula.