SERIKALI YATOA WITO KWA WADAU KUTUMIA VYEMA TAARIFA ZA HALI YA HEWA ZINAZOTOLEWA NA TMA


Na Mwandishi Wetu

Serikali yatoa wito kwa wadau wote kutimia vyema taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya  hali ya hewa Nchini kwa ajili ya kupanga shughuli za kiuchumi na kijamii na kufanya maamuzi , pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya Nchi


Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete alipokua akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya hali ya hewa duniani yenye kaulimbiu "mustakabali wa hali ya hewa , tabia ya nchi na maji kwa vizazi vyote" (the future of weather , climate and water across genereations). 


Mwakibete amesema kuwa utoaji wa huduma za hali ya hewa nchini ulianza kabla ya uhuru ambapo upimaji wa hali ya hewa ulianza mwishoni mwa miaka ya 1800 ambapo kituo cha kwanza cha hali ya hewa kilianzishwa mwaka 1892 katika mji wa Bagamoyo.


Aidha Naibu Waziri Mwakibete ametoa wito kwa wadau wote kutumia vyema taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini kwaajili ya kupanga shughuli za kijamii na kiuchumi na kufanya maamuzi pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi.


Akizungumzia tatizo la kimbunga lilizozikumba nchi jirani Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang'a amesema kuwa hali ya hewa haina mipaka hivyo mamalaka hiyo imekua na ushirikiano wa kimataifa kuhusu matukio ya hali mbaya ya hewa ili kuendelea kutoa elimu kwa jamii na kuchukua tahadhari.
Previous Post Next Post