BALOZI BOER APONGEZA MCHAKATO WA MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI NCHINI


Na Humphrey Msechu

Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania, Wiebe de Boer amepongeza mchakato wa mabadiliko ya Sheria ya Habari unaoendelea nchini.


Balozi Boer amesema hayo jana wakati alipotembelewa na Viongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), katika ofisi za ubalozi wa nchi hiyo, jijini Dar es Salaam.

“Nawapongeza kwa mchakato mabadiliko Sheria ya Habari. Mambo huenda taratibu,” Balozi Boer.



Ikumbukwe kuwa Februari 10 mwaka huu serikali iliwasilisha Bungeni muswada wa mabadiliko ya sheria ya Habari kupitia mabadiliko ya sheria mbalimbali. 


Muswada huo wa sheria ya huduma za habari unategemewa kusomwa tena kwa mara ya pili katika mkutano wa 11 wa Bunge ambao utaanza mwezi ujao.
Previous Post Next Post