HAKIELIMU WAMEPENDEKEZA DHANA YA ADHABU CHANYA KUPEWA MKAZO KWA WALIMU ILI KUEPUKA ADHABU ZA KIKATILI


Na Lilian Ekonga

Kufuatia Kifo cha cha Mwanafunzi Gloria Faustine (14) wa kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Mwinuko jijini Mwanza aliyeangukuwa na jiwe wakati akichimba kifusi kama sehemu ya utekelezaji wa adhabu aliyopewa baada ya kuzungumza kiswahili mazingira ya shule, Shirika la HakiElimu wamependekeza dhana ya adhabu chanya kupewa mkazo katika mafunzo tarajali na kazini kwa walimu ili kuwasaidia kuepukana na matumizi ya adhabu za kikatili. 

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Machi 22 Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu , Dkt James Kalage amesema shirika hilo limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kufariki wa Gloria na kusisitiza matukio kama haya ya adhabu zinazoleta matokeo hasi yanazidi kuongezeka na kuibua hofu kwa shule zetu na sio salama sana kwa watoto.


Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu Dkt. John Kalage amesema walimu wanajukumu la kuwafundisha na kuwajenga wanafunzi katika mwenendo unaofaa na jukumu hili wanaweza kulitekeleza kwa kutumia mbinu mbinu mbalimbali ikiwamo utoaji wa adhabu chanya ambazo zitasaidia kufikia malengo ya utoaji wa adhabu. 

"Tunapenda kusisitiza kuwa, adhabu zitolewazo kwa wanafunzi ni lazima zizingatie sana aina ya kosa au tabia inayokusudiwa kurekebishwa, na zilenge katika kumsaidia mtoto kuwa bora zaidi badala ya kumuumiza na kumwongezea hofu". Amesema Dkt.Kalage. 

Amesema kuwaadhibu wanafunzi kwasababu za kitaaluma kama vile kushindwa kuzungumza kiingereza, kuandika au kukokotoa kwenye hisabati hakuwezi kutatuliwa kwa kumpa mwanafunzi adhabu ambayo haimwelekezi katika kujifunza kile anachotakiwa. 

"Katika mazingira haya, mwalimu angeweza kuagiza wanafunzi waandike insha ya lugha ya Kiingereza, kusoma vitabu vingi vya hadithi za Kiingereza na kutoa tafsiri". Amesema 

Pamoja na hayo Hakielimu imetoa rai kwa Serikali kurejea upya mapendekezo yanayotolewa na wadau kuhusu matumizi ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia ngazi ya Sekondari. 

Dkt.Kilage amesema wanafunzi wanaotoka shule za msingi na hasa za umma kuingia kidato cha kwanza, wanakuwa hawajawa tayari kuweza kutumia lugha ya Kiingereza katika kuzungumza na kujifunzia.
Previous Post Next Post