MAONI YA WADAU WA HABARI BAADA YA MUSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA YA HABARI KUWASILISHWA BUNGENI


Na Humphrey Msechu,

Wadau mbalimbali wa Habari Nchini wametoa maoni yao kuhusu muswada wa mabadiliko ya sheria ya habari baada ya Serikali kuwasilisha muswada huo tarehe 10 Februari mwaka huu kwenye mkutano wa 10 wa Bunge.

"Wakili wa kujitegemea amesema kuwa sasa ni jukumu letu kuangalia vile vipengele tulivyotaka vibadilishwe vimefanyiwa kazi
Serikali imeishatoa mapendekezo, sasa ni jukumu letu kuangalia vifungu tulivyokuwa tunataka vibadilishwe vimefanyiwa kazi? Kama bado tunatakiwa kupeleka mapendekezo kwa kamati husika ili muswada ukirejeshwa bungeni, wabunge wawe na mapendekezo yaliyoshiba"- James Marenga, MISA TAN

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Nchini Deodatus Balile amesema kuwa kuna uwezekano wa kupata sheria nzuri ya habari kama wadau wataungana na kushirikiana.

"Sheria ikiwa nzuri kila mmoja wetu atafurahi, kila sekta itakuwa. Bado tuna nafasi ya kujadili kwa kina (Muswada wa Habari )" - Balile.
Ni matumanini ya wadau wengi tasnia ta Habari itapata sheria nzuri za habari mara baada ya muswada wa mabadiliko ya sheria ya Habari kupitishwa Bungeni.

Previous Post Next Post