Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Maendeleo la Taifa(NDC) limewashauri wanawake nchini kutumia dawa ya kuuwa viwadudu vya mazalia ya mbu ili kuweza kupambana na ugonjwa wa Maralia nchini.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam Afisa Rasilimari watu wa Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC),Vailentine Simkoko wakati zoezi la kunyunyiza viwadudu kwenye mazalia ya Mbu mabibo relini ,ambapo zoezi hilo limefanywa na wanawake wa NDC ikiwa ni sehemu ya jamii kuelekea maazimisho ya siku ya wanawake Duniani marchi 8 mwaka huu.
Simkoko amesema wameamua kuanzisha zoezi hilo ni kufuatia kubainika wanawake wanaathirika za ugonjwa wa Maralia.
"Tunapoua mazalia ya Mbu yanasaidia kutokomeza ugonjwa wa maralia ambao umekuwa ukiwaathiri wanawake hasa wa mama wajawazito na tunawashauri wanawake watumia viwadudu vinavyotengenezwa kiwanda cha viwadudu kibaha mkoa wa pwani' Amesema Simkoko.
Naye mratibu wa zoezi hilo,Ester Mwaigomela amesema wanawake wa NDC wameafua kujikita katika zoezi hili katika eneo la Mabibo relini ni kuhukikisha wanatokomeza ugonjwa wa maralia katika eneo hilo.
Kwa upande wake,Abedi Mbonde,ambaye ni mjumbe wa serikali za mtaa Mabibo jijini Dar es Salaam ameishukuru NDC kwa zoezi walilolifanya na kuwataka kuwa endelevu maeneo mbalimbali ili waweze kutokomeza ugonjwa wa maralia nchini.