WANANCHI WAASWA KUWASILISHA MALALAMIKO YA RUSHWA KWA TAKUKURU NA SI VINGINEVYO


Na Lilian Ekonga, DAR ES SALAAM 

Takukuru mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam imetoa wito kwa wananchi wa eneo hilo kuwasilisha malalamiko katika ofisi hiyo yanayoangukia kwenye sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 na sio malalamiko yasiyohusu sheria hiyo.

Wito huo umetolewa na Naibu mkuu TAKUKURU mkoa wa Temeke Eugenius Hazinamwisho wakati akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha robo ya Oktoba hadi Disemba mwaka 2022 ambapo imepokea malalamiko 41 huku 36 yakihusu rushwa na matano hayahusu rushwa.

"Taarifa 36 zinazohusu rushwa zilihusu sekta au maeneo ya WEI 1, Ardhi 05, Binafsi 13, Manispaa Temeke - Ugavi 1, Elimu 06, TRA 01, Mahakama 03, Soko 1, ORYX1, TIPER 1 Polisi 1 na Michezo1" amesema Hazinamwisho.

Aidha katika uziaji rushwa taasisi hiyo imeshirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Temeke imefuatilia utekelezaji wa miradi tisa yenye thamani zaidi ya Shilingi bilioni 5 inayohusu sekta ya elimu, afya pamoja na miradi ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko19.

Ameongeza kuwa katika robo ya Januari hadi Machi mwaka huu taasisi hiyo inaimarisha juhudi za kuzuia rushwa kw kuongeza ushiriki wa kila mwananchi na wadau katika kukabiliana na tatizo la rushwa katika utoaji wa huduma za jamii na kuhamasisha ushiriki katika vita dhidi ya rushwa.

Pia amesema wataendelea kufuatilia makusanyo na uwasilishaji wa mapato yanatokana na mashine za POS na kuchukua hatua stahiki kwa wale watakaobainika kufuja mali za umma.
Previous Post Next Post