Na Mwandishi wetu
CHAMA Cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) kimeingia mkataba wa makubaliano na Kampuni ya The Marketing Changer Limited(TMC) kwa ajili ya maendeleo ya Mchezo wa Baiskeli utakakuwa wa miaka mitano.
Akizungumza jana jijini Dar eS Salaam Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Arnold Kileo,,alisema kuwa mkataba umelenga kukuza hadhi ya mchezo hapa nchini.
Alisema kuwa kampuni hiyo itashirikiana na Wadau na mashirika mbalimbali na kuweka mipango na kushindanisha watu Ili waweze kuboresha afya zao na kusaidia kutengeneza timu ya taifa.
" Tunatarajia kuandaa matukio mbalimbali yakiwamo ubingwa wa taifa mwaka huu ambalo litafanyika mwezi Juni mwaka huu na kufuatiwa na lingine lijulikanalo Mwanza Open Cycle Challenge 2023," alisema Kileo.
Kwa upande wa Rais wa CHABATA Godfrey Jax Mhagama,alisema kuwa TMC watakuwa wakala halali kisheria kufanya Kazi na Chama katika kutafuta wadhamini
Alisema kuwa ,kuwa mshauri kimasoko,kusimamia haki za kujitangaza za wadhamini,kusimamia mipango na makubaliano na waandaaji na kusimamia shindano la ubingwa wa taifa.
"Ushirikiano huu utakuza na kuhamasisha zaidi mchezo wa Baiskeli ambao kwa kiwango fulani umekuwa na ufifiaji Kwa kipindi hili ,hivyo watakauwa wakala halali wa chama katika kusimamia maendeleo ya mchezo huu," alisema Mhagama.
Aliongeza "tumefurahi kupata Hawa tutaingia mfumo wa Chama cha kimataifa ambao waliacha na wanatumia wakala ambao wanautaalaam wa kuongea tutapata faida kubwa ," .