WENYE KIFUA KIKUU NA VVU KUPATA ELIMU YA LISHE KIGANJANI


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wamezindua Programu ya Simu inayohusu Masuala ya Lishe kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI pamoja na kifua kikuu ili kusaidia kukabiliana na magonjwa nyemelezi na kuimarisha hali zao za lishe.

Akizundua Programu hiyo Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumaini Nagu amesema programu hiyo itaongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na magonjwa hayo na ikiwezekana kuyatokomeza kabisa.


Programu hiyo kwa sasa itapatikana kwenye simu zenye mfumo wa Android na baadae kwenye simu zenye mfumo wa IOS na ambayo itamuwezesha mgonjwa wa kifua kikuu na mtu anayeishi na ugonjwa wa UKIMWI kumwezesha kupata erlimu yam lo kamili kupitia video na majarida mbalimbali pamoja kujfanyia tathmini ya hali yake la lishe.

"Lishe hii ni moja ya mikakati ya kuwajengea wananchi uelewa kuhusu masuala ya lishe bora na kuchochea mfumo bora wa lishe,kupitia programu hii naamini Itasaidia kutoa elimu na ujuzi namna ya kuandaa milo na kutumia vyakula vinavyopatikana katika maeneo husika, Hii Itasaidia kufikia malengo ya wizara ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yale yasiyo ya kuambukiza,"amesema Prof Nagu.


Ili kufanikisha malengo ya serikali, Profesa Nagu ameitaka TFNC kuihakikisha kupitia Programu hiyo inawafikia watu wengi zaidi wakiwamo wenye magonjwa ya Kisukari na Saratani


Makundi mengine aliyoagiza Profesa Nagu yafikiwe ni watoto wadogo, wachanga,vijana balehe; wajawazito na wanawake wanaonyonyesha pamoja na; makundi mengine ili kuongeza chachu ya mabadiliko chanya katika ulaji unaofaa na mitindo bora wa maisha.


Pia ameiagiza taasisi hiyo kubuni njia za kuwafikia wanaume ili kuleta uelewa wa pamoja katika familia kwa lengo la kukinga badala ya kutibu.



Previous Post Next Post