MAADHIMISHO YA SIKU YA UHANDISI DUNIANI KUTOA FURSA NA KUTHAMINI MCHANGO WA UHANDISI


Na Judith Chao, Dar es Salaam

Taasisi ya wahandisi Tanzania (IET) imetangaza
maadhimisho ya siku ya Uhandisi duniani yanayo fanyika kila tarehe 4 Machi ya kila mwaka yenye lengo na madhumuni ya kutoa fursa ya kutambua na kuthamini machango wa uhandisi na watekelezaji wa kazi za kiuhandisi nchini. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 3, Rais wa Taasisi ya wahandisi Tanzania, Dkt Gemma Modu amesema Maadhimisho hayo yatafanyika siku ya kesho katika viwanja vya karemjee jijini Dar es salaaam.

Amesema tarehe 4 Machi 2023 ,Taasisi ya waandishi Tanzania(IET), ikishirikiana na chama cha wahandisi Washauri Tanzania (ACET) na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) zitaungana na taasisi zote za Kihandisi Duniani kupitia shirikisho lq Taasisi za Kihandisi la Afrika Mashariki(EAFCEO) na shirikisho la Taasisi za Kihandisi la Afrika(FAEO) kuadhimisha siku hii.

"Wahandisi na mafundi wote katika kuleta maendeleo endelevu ya taifa letu na dunia kwa ujumla, kuboresha uelewa wa umma kuhusu jinsi ya uhandisi na teknolojia vilivyo na umuhimu kwa maisha yetu ya kila siku katika ulimwengi wetu wa sasa"amesema Dkt Modu.

Ameongeza kuwa Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 200 kutoa taasisi mbalimbali za umma na binafsi huku kauli mbiu ikiwa Ubunifu wa Uhandisi kwa ulimwengu unaostahimili zaidi.

Aidha amesema taasisi zitakazoshiriki zitapata fursa ya kuonyesha ubunifu katika kutekeleza mirafi mbalimbali ya kimkakati inayoendelea hapa nchini na kazi mbalimbali za kiuhandisi.

" Pamoja na washiriki ambao watapata fursa ya kuzungumzia yale wanayofanya kwenye miradi yao, pia tumewaalikw wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo ili waweze kuonyesha uwezo wa ubunifu wao katika ngazi za masomo na vilevile kuona na kujifunza yale yanayofanyika kwenye miradi ya taifa ya kimkakati, amesema Dkt Modu.
Previous Post Next Post