JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM LIMEANDAA MBIO ZA PUGU MARATHON KUSAIDIA UKARABATI KUTUO CHA HIJA


Na Lilian Ekonga, Dar es Salaam

Jimbo kuu la Dar es Salaam limeandaa mbio za Hisani ambazo zitatambulika kama Pugu Marathon zenye lengo la kusaidia kupata majitoleo kwa ajili ya kuendeleza kituo cha Hija kinachopatikana Pugu na Kukarabti Nyumba aliokuwa akiishi Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopo Pugu Sekondari. 

Hayo yamesemwa na Askofu wa wa Jimbo kuu la Dar es salaam Jude Thaddaeus Ruwa'ichi,  wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema Mbio hizo zitafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 27 Mei 2023 kuanzia saa 12 asubuhi. 

"Matembezi ya kilomita 2 ada ya ushiriki 20,000, Mbio fupi za kilomita 5 ada ya ushiriki 20000 , Mbio za kilomita 10 ada ya ushiriki 30000,Mbio za kilomita 21 ada ya ushiriki 30000",amesema. 

Pia amewaomba wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi katika mbio hizo, mashirika, Makampuni, wafanyabiashara ma wadau wengine kujitokeza kwa kufadhili ili waweze kufanikisha lengo kuu la mbio hizo.

Ameongeza kuwa jinsi ya kushiriki katika Mbio hizo,Mshiriki anaweza kujisali katika ukurasa wa google wa Jimbo kuu la Dar es salaam ambapo atakutana na fomu ya kujaza taarifa zake ikiwemo aina ya mbio atataka kushiriki, majina, namba za simu na baadae atapokea masage ya ambayo atatumiwa number kwa ajili ya kufanya malipo.

"Mapato tutakayo pata yatasaidia kukarabati kituo cha Hija Pugu, nyumba aliyokuwa anaishi hayati Mwalm julius Kambarage nyererere iliyokuwa Pugu sekondari na tunatarajia kukusanya shilingi milioni 400" amesema.
Previous Post Next Post