RAIS SAMIA KUWA MGENI RASI KATIKA MASHINDANO YA MAKUBWA YA QUR' AAN TUKUFU AFRIKA


Na Lilian Ekonga, Dar es salaaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Mashindano makubwa ya QURAN tukufu Africa kwa 2023 yatakayofanyika kwenye uwanja wa uhuru jiji Dar es salaam siku ya tarehe 9 mwezi nne mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa mashindano hayo Sheikh Nurdeen kishk alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo yaliofanyika leo Aprili 4 jiji Dar es salaam.


Sheikh Kishki amesema mashindano hayo yataunganisha nchi 23 barani Afrika na washiriki 24 kutoka kila nchi huku mshiriki mmoja w akitoka katika taasis ya Al -Hikma faundation ambao ndo wasimamizi wa mashindano hayo.

"Kuna washiriki wengine watatu watatoka katika bara la Asia, Amerika na Ulaya ambao wao watashiriki kama washiriki Maalumu na hawa hawataungana na washiriki 24 kutoka bara la Afrika"amesema sheikh Kishki.

Pia ameongeza kuwa zawadi zitakazo tolewa kwa mshindi wa kwanza wa bara la Afrika atapewa kiasi cha shilingi dola Elfu 10 sawa na shilingi milioni 25 za kitanzania na kwa waupande wa Mshindi kutoka washiriki maalumu wa mabara matatu atapewa Dola elfu 5.


Kwa upande wake Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Abubakari bin Zuber bin Ally, ameipongeza taassi ya Al-HKMA kwa kuanzisha mashindano hayo ya QURAAN na kufarahia idadi ya watu watakao kuja kushindana na zawadi zitakazo tolewa.

Pia Sheikh Mkuu amesisitiza kwa upande wa zawadi wazazi na walimu nao waweze kupewa zawadi kwakuwa wao wanamchango mkubwa kwa washiriki hao watatokuja kushiriki hasa kwa yule mshindi atakaye pewa zawadi.

Aidh amesisitiza swala zima la maadali hususani ndoa za njinsia moja ziweze kukomeshwa kwani ziharabu mwendeno wa watu na kuwaomba masheikh kuhakikisha wanakemea ipasavyo kuhakikisha swala hilo linakwisha kwakuwa hata dini hairuhusu maswala hayo.
Previous Post Next Post