LHRC WAOMBA UCHUNGUZI WA KINA UFANYIKE UTATA WA KIFO CHA MTUHUMIWA WA UGAIDI


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam

Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC kimeishauri Tume ya Haki Jinai inayoendelea na zoezi la ukusanyaji maoni nchini kutumia fursa hiyo kutoa mapendkezo kwa Rais juu ya watuhumiwa wote wa makosa ya ugaidi waliokaa mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kesi kusikilizwa ili Mkurugenzi wa mashtaka DPP kuwaachia huru.

Ushauri huo wa LHRC kwa kushirikiana na Jumuiya na taasisi za Kiislam umekuja mara baada ya taarifa ya kifo cha Sheikh Saidi Mohammed Ulatule kilichotokea Machi 4 mwaka huu aliyekuwa akituhumiwa kwa ugaidi ambapo aliwekwa gerezani tangu mwaka 2016.


Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Anna Henga ameshauri mwendesha mashtaka wa serikali awafutie mashtaka au awafikishe mahakamani kwa mujibu wa kifungu cha 91 cha sheria ya Mwenendo wa Mashauri ua jinai.

"Serikali iwaachilie huru au iwape hakinya kijitetea mahakamani watuhumiwa wote waliokaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja bila ya mashauri yao kusikilizwa" amesema Anna Henga.


Kwa upande Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Sheikh Ponda Issa Ponda pamoja na mmoja wa Familia ya marehemu Ulatule Mohammedi Saidi, wameiomba serikali kufanya marekebisho ya sheria za vyombo vya dola pamoja na kutoa haki kwa mahabusu waliokaa muda mrefu gerezani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 10 mwaka huu na Mkuu wa Magereza Dar es Salaam, George Wambura amesema kifo cha sheikh huyo kilichotokea Machi 4, mwaka huu, kimetokana na ugonjwa wa shinikizo la moyo uliokuwa unamkabili tangu mwaka 2017 alipoingia gerezani.
Previous Post Next Post