RAIS SAMIA MGENI RASMI MASHINDANO MAKUBWA YA QUR'AAN NCHINI


Na Mwandishi Wetu

Waandaaji wa Mashindano Makubwa ya Quran Tanzania Shekh Nurdeen Kishki, Shekh Othman Kaporo na Bi Aisha Sururu wametoa Taarifa ya Mashindano ya Quran Mwaka huu ambapo ya kitaifa Yatakuwa Tarehe 2 katika Ukumbi wa Diamond Chini ya Taasisi ya Bi Aisha Sururu Foundation.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Taasisi ya Aisha Sururu u faundation, Bi Aisha sururu amesem mgeni rasmi wa mashindano ya kitaifa atakuwa Rais Samia suluhu Hassan na mashindano yataanza kuanzia saa 12 hasubuhi.
 

Bi aisha ameongeza kuwa mashindano hayo watahudhuria watanzania wate pamoja na visiwani humu akiwakaribisha watu kuweza kujitokeza katika mashindano hayo.

Kwa upande wake Shekh Nurdeen Kishki mwenyekiti wa alhkima foundation ambao wanasimamia mashindano ya Afrika yatakayo fanyika tarehe 9 ya mwezi wa nne katika viwanja vya Uhuru jijin dar es saalam huku akiwaalika waslamu na watanzania wote huku wakishukuru wazira kwa kuwaunga mkono katika mashindano hayo.



"Mgeni rasmi katika mashindano haya ni Rais Samia Suluhu hassan na kauli mbiu yetu ni allah ana anawatu na watu wake ni wa QURAN"

Nae Shekh othuman Kaporo mwenyekiti wa jumuhiya ya kuhifadhisha QURAN ambao wanasimamia tuzo za mashindano Dinunia amesema mgeni rasmi katika mashindano hayo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi yatayofanyika tarehe 16 ya mwezi wa nne katika Ukumbi wa diamnond jubilee.

"Tunawaalika wepenzi wa QURAN na watanzania wote huku kauli mbiu yetu ikiwa QUORAH ni chimbuko la maadili, maadili yamekuwa hovyo watu wanakataa maumbilie yalioubwa Mungu sisi katika mwaka huu tutapiga kelele kuhakikisha tunarekebisha maadili" amesema Shekh Kaporo.
Previous Post Next Post