NDC YAINGIA MAKUBALIANO NA TEMDO


Na Lilian Ekonga, Dar es Salaam

Shirika la maendeleo la Taifa NDC limeingia makubaliano ya ushrikiano na taasisi ya uhandisi na usanifu wa mitambo TEMDO katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la utafiti , kubadilishana ujuzi pamoja na kuongeza uzalishaji katika kiwanda cha Kilimanajro Machine Tools 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa makubaliano hayo Mkurugenzi mkuu wa shirika la NDC Nicolaus Shombe amesema kuwa makubaliano hayo yatasaidia kuongeza ufanisi katika uzalishaji pamoja na kupunguza gharama za kuagiza mitambo kutoka nje ya nchi.

Ameongeza kuwa TEMDO wanauwezo wa kuzalisha mitambo sita kwa mwaka hivyo kwa kushirikiana nao wataweza kuzalisha mitandambo mingi na kuuza mpaka nje nchi ya Tanzania. 


"Eneo kubwa kuliko yote ni eneo la utaalamu sisi ambapo wataalamu wetu wanaweza kufanya kazi TEMDO na wao wakaja kwetu kufanya kazi na kujifunza vitu mbalmbali" amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya uhandishi na usanifu wa mitambo TEMDO Profesa Fredrick Kahimba amesema matarajio ya mashirikiano katika taasisi hizo mbili ni pamoja na kuongeza ubora wa bidhaa , kupunguza matumizi ya fedha za kigeni na kuzalisha ajira kwa watanzania 

"Kwa kushirikiana na kilimanjaro Mashine tools(KMTC)tutaweza kutengeneza minara ya umeme ambayo tulikuw tunanunu kwa bei ya juu sana nje ya nchi, lakin pia itakapotaka kutengenezwa tutakuwa tunatengeneza hapa hapa kwaiyo tutakuwa tumeisaidia serikali kwa kiwango kikubwa sana" amesema professa Kahimba
Previous Post Next Post