NAIBU WAZIRI HAMISI MWIJUMA ATOA MAAGIZO KWA BAKITA KUHAKIKISHA TUNAJIMILIKISHA KISWAHILI


Na Lilian Ekonga.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamisi Mwijuma ametoa Maagizo kwa Baraza la Kiswahili Tanzania(BAKITA) kuhakikisha tunajimilikisha kabisa lugha ya kiswahili kwa kuwa viongozi kila linapokuna jambo linahusiana na Lugha ya Kiswahili.

Hayo ameyasema wakati alipotembelea Ofisi za BAKITA leo Machi 17 jijini Dar es salaam ambapo amesema Tanzania tuwe wa kwanza kokote duniani linapokuja swala la kuzungumza Kiswahili.


Naibu Waziri ameongeza kuna balozi 9 tayari kumewekwa vituo kwaajili ua kufundishia lugha ya kiswahili na lengo ni kuhakikisha kiswahili kina sambaa zaidi na watu wengi waweze kukiongea kiswahili halisi cha Kitanzania.

Pia amesema wanatengeneza kanzi data ya wataalamu wa ufundishaji wa kiswahilu lengo likiwa ni kuwa na kanzi ambayo inatatoa wataalamu wa kwenda kufundisha maeneo mbalimbali na kufanya tafsiri kutoka lugha nyingine kuja kiswahili. 


"Tunampango wa kuweka wataalamu mpaka watakao weza kutafsiri kichina kuja kiswahili na kiswahili kwenda kichina ,Lengo kubwa ni kujimirikisha kiswahili na kifahamike kuwa lugha kutoka nchi ya Tanzania"amesema Naibu waziri.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Baraza la kiswahili Tanzania (BAKITA) Consolatha Mushi ametoa Rai kwa Watu wanaotumia kurasa za BaKITA kuandika maneno ambayo hajatafsiriwa na BAKITA kuacha mara moja kutumia kurasa hizo kwa wanaiposha jamii.
Previous Post Next Post