Na Lilian Ekonga
WAANDAJI wa filamu na tamthilia nchini wameombwa kuzidisha ubunifu katika hadithi wanazoziwasilisha kwa lengo la kuleta ushindani sokoni.
Hayo yameswa leo January 9 na Mkuu wa Channel ya Sinema Zetu kutoka Azam Tv, Sophia Mgaza katika uzinduzi wa tamthilia mbili ya Zahanati ya Kijiji na Fungu Langu ambazo zilizinduliwa jana katika hoteli ya Tiffany.
Zahanati ya Kijiji itaanza kuruka leo saa 1 usiku ambayo ipo chini ya Nabra Creative Company Limited, Abdul Usanga na Fungu Langu chini ya J-Film 4Life chini ya Jeniffer Kyaka 'Odama'
Sophia amesema wasanii wanapaswa kufanya uwekezaji mkubwa ambao unaendana na kazi wanazowalisha watazamaji na jamii.
"Filamu na tamthilia ni biashara hivyo wasanii mnapaswa kuongeza ubunifu wa maudhui katika kazi mnazozifanya, "amesema
Msanii mkongwe wa filamu nchini, Jacob Stephen amesema kila mwaka tamthilia zinazidi kuwa bora kutokana na ubunifu wa waandaji wa kazi hizo.
"Ombi langu kwa waigizaji wa zamani kurudi tena kwa lengo la kuongeza nguvu katika tasnia na kusaidia na wasanii wachanga, " amesemaJB.
Tamthilia ya 'Zahanati ya Kijiji' imeanza kuonyeshwa jana huku 'Fungu Langu' inatarajiwa kuanza Januari 20 mwaka huu.