KISHIMBA AIPA TANO SERIKALI YA RAIS DKT. SAMIA KUTOA TANI 1000 ZA MAHINDI KWA WANANCHI WA JIMBO LAKE


Na  Mwandishi Wetu, Kahama 

MBUNGE wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba amesema kuwa wameanza kupokea mahindi Kwa ajili ya chakula na tayari Tani 100 za mahindi zimeshapokelewa na wataendelea kupokea Tani zingine zipatazo 1000.ambazo zitasaidia wananchi Kwa kipindi hiki ambacho bado Kuna changamoto ya chakula.

Amesema kuwa wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta Mahindi hayo Kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kupata chakula kitakachowasaidia wananchi Kwa kipindi hiki ambacho  wanauhitaji wa chakula uku wakijiandaa kwenda kuvuna mazao miezi ijayo.



Kishimba ameyasema hayo wilayani kahama wakati akishuhudia wananchi wakinunua Mahindi Kwa Bei elekezi ya Serikali ya shilingi 15000 Kwa debe Moja lenye ujazo wa kilo 20. Ambapo amesema kuwa Bei hiyo inaweza kusaidia kupunguza mfumuko wa Bei mitaani  hususani kwenye maeneo ya Lunzewe,katoro mkoani Geita pamoja na Kagongwa wilayani humo ambalo wanalima Mahindi Kwa wingi.

"Tunaomba wananchi wa maeneo mengine ambako wataanza kupeleka Mahindi Siku chache zijazo wawe wavumilivu lakini pia kama wataweza kuja hapa kahama Mjini nawaje "amesema Kishimba 

Mbunge huyo amekiri,kwamba hali ya chakula Kwa wananchi wa Jimbo ilikuwa mbaya sana kwasababu debe Moja la Mahindi lilikuwa linauzwa Kwa Bei ya shilingi 25000 ambayo ni Bei ya juu kabisa kuwahi kuishuhudia ambapo Mahindi ya Serikali yanauzwa Kwa Bei ya shilingi 15000 Kwa debe sawa na nusu ya Bei ya awali.



Amesema kuwa baada ya Serikali kuleta ahueni ya Bei ya Mahindi Kwa wananchi hivi mitaani Bei umeanza kupungua na hiyo ni baada ya wafanyabiashara kugundua kuwa Serikali imeanza kuleta  Mahindi Kwa wananchi wake.

"Kutokana  na hali hii tunatarajia inaweza kutusaidia kabla hatujapata chakula kingine Kwa maana ya kuvuna hivyo tunaendelea kuwahimiza wananchi wajikite zaidi kwenye uzalishaji hasa wakati huu ambapo inaonekana kama mvua zinaendelea kunyesha na kwasababu wananchi wajimbo hili ni wachapa kazi."amesema Kishimba 



Ameongeza kuwa wananchi hao ni wazalishaji wazuri wa mazao ya Mahindi ,karanga ,mpunga na mazao mbalimbali na wakati wowote ndani ya wiki zijazo baadhi ya mazao yataanza kuvunwa  kwahiyo tatizo la njaa litapungua kwa kiasi kikubwa.



Hata hivyo akizungumzia  ruhusa ya mikutano Kwa vyama  vya upinzani amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuviomba vyama vyote nchini kutumia fursa hiyo kuelezea mazuri yanayofanywa na Serikali lakini pia kueleza sera zao mbele ya wananchi.


Previous Post Next Post