Mgodi wa CANUCK kutoa ajira lukuki kwa wakazi wa Kahama


 

Na Mwandishi Wetu,

 

 

IMEELEZWA kuwa wakazi wa Kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamenufaika na ajira kutoka katika Mgodi wa CANUCK uliopo kwenye Kijiji chao.

 


Hatua hiyo imeelezwa na meneja wa Mgodi huo David Deogratius alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake na kwamba kwa sasa Mgodi huo umeweza kutoa ajira za kudumu kwa wafanyakazi 270 na umeendelea kuongeza idadi ya wafanyakazi 51 ambao wanakwenda kuaza kazi katika idara ya (MINING) na idara ya uzalishaji kuongeza wafanyakazi 35.





Ameongeza kuwa kwa mwaka 2021 /22 waliweza kukaa na serikali ya kijiji licha ya kwamba ndio wameaza kazi lakini walikubaliana kutenga kiasi cha fedha shilingi milioni 30 kwa lengo la kusaidia shughuli za maendeleo na miradi bunifu ambayo itaibuliwa na serikali ya kijiji na wamekuwa wakifanya hivyo mfano katika milioni 30 ya mwaka huo kampuni iliweza kulipa shilingi milioni tano katika ununuzi wa ardhi kwa ajili ya matumizi ya kujenga kituo cha afya cha kijiji cha Magung'humwa na hivi karibuni kampuni imeweza kulipa kiasi cha shilingi milioni 7.5 ili kusaidia ujenzi wa jengo la kituo cha afya.

 


 

Meneja huyo  ameongeze kuwa kutokana na uzalishaji wameazisha zamu tatu kwa wafanyakazi na wanahitaji wafanyakazi 70 hadi 100 hivyo kwa kiwango cha chini Kampuni inatarajia kuwa na wafanyakazi 350 mpaka 400 na hadi kufikia sasa anawafanyakazi 270.

 

wakati huohuo amesema kuwa kampuni yao ilipewa leseni ya uchimbaji lakini ndani ya leseni hiyohiyo kuna uvamizi wa wachimbaji wadogo ambao wanatambua kabisa kuwa Kampuni ya CANUCK ilishapewa leseni ya uchimbaji  lakini kwa kuzingatia mahusiano wanaomba mamlaka husika kuliangalia suala hilo na kuweza kupata ufumbuzi mapema kabla ya wale watu hawajafanya uwekezaji mkubwa ambao unaweza kuathiri uzalishaji.

 


Amesema kuondoka kwa watu hao kutawezesha kampuni kuweza kuongeza uzalishaji kwa maana uwezo wa kampuni kuzalisha zaidi  kwani kushoto kwa mgodi wao kuna leseni ya watu wengine na kulia pia kuna leseni ya watu wengine na mbele yao kuna wachimbaji wadogo ambao wamevamia hivyo wanajikuta wako katikati na wanashindwa kujitanua ukizingatia leseni yao imefika hadi huko.

 

"Niombe pia kupaza sauti kwa serikali kupitia Wizara ya Madini ,keweza kusadia kulisukuma jambo hili japo kuwa tunapata ushirikiano mzuri kutoka kwa kamishna mkazi wa mkoa wa kimadini  Kahama na mkuu wa wilaya ya kahama Festo Kiswaga lakini tunaamini tutafanikisha kwa wakati hali ambayo itaongeza uzalishaji  na tukiweza kuzalisha zaidi tutaweza kurudisha kikubwa kwa jamii inayotuzunguka katika mfuko wa CSR ."amesema Deogratius      

 

 

Mneja huyo rasirimali watu na utawala wa Kampuni ya Mgodi wa CANUCK amesema kuwa kampuni hiyo ilipata leseni ya uchimbaji wa madini katika kijiji hicho mwaka julai 30 mwaka 2020  na baada ya kupata leseni hiyo waliaza shughuli za uchimbaji wa madini mara moja.

 

Amesema kuwa mwezi semptemba mwaka 2020 waliaza kuwasha mitambo na majaribio ya shughuli za uchakataji wa dhahabu na hadi sasa wanaendelea na shughuli hizo za uchimbaji wa madini ya dhahabu.

 

 

Amesema kuwa wanafanya hivyo ikiwa ni sehemu juhudi zinazofanywa na jamii  katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ndani ya kijiji hicho ambayo wanayaazisha lakini pia licha ya kijiji hicho pia wamekuwa wakisaidia kwenye ujenzi wa maendeleo kwenye vijiji vingine ndani ya wilaya hiyo hata kabla ya kuingia kwenye mfuko wa maendeleo (CSR)  na wanafanya hivyo kadri wanavyopokea maombi kutoka kwenye maeneo hayo.

 

Meneja huyo akitolea mfano wa moja ya vijiji ambavyo  vimeendelea kunufaika uwepo wa mgodi huo ni pamoja na kijiji cha Numbwi ,kagongwa na isaka kote huko walipokea maombi ya kusaidia shughuli za maendeleo ikiwamo ujenzi wa mashimo ya vyoo vya wanafunzi katika shule ya msingi Numbi ilipo katika kijiji cha Numbi na katika kata ya isaka kuna ujenzi wa kituo kipya cha polisi kampuni ya CANUCK baada ya kualikwa kama wadau wamaendeleo waliweza  kufika na kuchangia  nondo 70, lakini mbali na hapo kampuni hiyo wameweza kuweka miundombinu ya maji safi na salama eneo linalozunguka mgodi kwa ajili ya wananchi kuweza kupata huduma hiyo bure.

Previous Post Next Post