OFISI YA MUFTI YATOA MSAADA KWA WATU MWENYE UHITAJI MAALUMU


Taasisi ya  Kuhudumia jamii chini ya Mkurugenzi wa  Da,awa na Tabligh Bakwata  Ofisi ya Mufti wa  Tanzania shekh Abubakar Zuberi, wemetoa msaada wa baskeli za walemavu 20, cherehani 20 na vifaa vya biashara 200 kwa watu wenye uhitaji  maalumu.

Akizungungu na waandishi wa  habari Mkurugenzi was Taasisi hiyo Arif Surya amesema vifaa walivyotoa vinadhamani ya milioni 80 kwa kushirikiana Taasisi mbali mbali za Misaada ndani na Nje na Nchi.

"Kwa ajili ya Mahitaji ya Kiroho tunafanikisha chakula Cha roho kupitia Ofisi ya Mufti kitengo Cha Da'awa na Tabligh na kushirikiana na taasisi zenye kazi hizo ndani na Nje ya Nchi ambapo tunaleta Mashekhe kutoka Nchi mbalimbali kwa ajili ya kufikisha Da'awa Mjini na Vijijini".amesema Arif Surya.

Aidha Amemshukuru Rais Samia Suluh Hassan kwa uongozi mzuri wa serikali wa awamu ya sita kwa kuwa kiongozi  mwenye huruma,upendo, uvumilivu, uadilifu na mwenye  uaminifu.

Salumu, mmoja wa watu waliokabidhiwa baskeli ya walemavu amesema wanamshukuru Mufti wa Tanzania sheikh Abubakar Zuberi kwa msaada alioutuo kwa watu wenye mahitaji maalumu.



"Niliambiwa Kuna Msaada na Mimi nilifika hapo  na kuweza kukabidhiwa baskeli ya walemavu"amesema salumu.

Taasisi ya Khidmatul Ummah yenye maana ya Kuhudumia jamii kwa mahitaji ya Kiroho na Mahitaji ya kimwili Ina lengo ya Kuhudumia wananchi kwa kutoa Misaada mbalimbali ambapo wanaleta Mashekhe kutoka Nchi mbalimbali kwa ajili ya kufikisha Da,awa Mijini na Vijijini Nchi nzima.



Previous Post Next Post