KAMATI KUU CCM YAIELEKEZA SERIKALI KUCHUKUA HATUA STAIKI KUHUSU MAONI YA WANANCHI KATIKA ENEO LA TOZO



Na lilian Ekonga

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imeielekeza Serikali kutazama hali halisi na kuchukua hatua stahiki kuhusu ushauri na maoni  ya wananchi katika eneo la Tozo za miamala ya kielektroniki, iliyoanza kutekelezwa hivi karibuni.

Hayo yamesemwa Leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, itikadi na uenezi, Shaka Hamdu Shaka Katika Ofisi ndogo ya makao Makuu y CCM jijini dar es  salaam.

Amesema  baada ya kutafakari na kujadiliana  kwa kina Kamati Kuu imeona umuhimu wa serikali kusikiliza maoni na ushauri wa wananchi kuhusu Tozo hizo.

Shaka amsema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea, kutafakari na kujadili kwa kina kuhusu hatua za kibajeti zinazoendelea kuchukuliwa kwa lengo la kupata fedha za kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kasi ili kuwawekea wananchi mazingira mazuri ya kujipatia maendeleo, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025.

"Eneo moja wapo ikiwa ni kupitia Tozo ambapo ni ukweli usiopingika kwamba serikali imeweza kufanya mambo makubwa katika kipindi kifupi kwa mfano; kama vile ujenzi wa vituo vya afya 234 na shule mpya za sekondari 214 na maeneo mengine kadhaa ambayo yanagusa maisha ya watanzania ya kila siku" Amsema Shaka.


Aidha amsema Kamati Kuu ya CCM imeelekeza Serikali kufikiria na kujielekeza katika kubana matumizi Serikali, kuendelea kujenga mazingira rafiki na wezeshi ili kujenga uchumi imara unaozalisha kwa lengo la kutanua wigo wa kodi pamoja na kubuni vyanzo vipya vya kodi ili kuwa na viwango pamoja na mfumo rafiki wa kodi kwa kila mmoja.

Pamoja na Hayo Shaka amesema Kamati Kuu ya CCM, imempongeza RAIS  Samia Suluhu Hassan kwa namna Serikali anayoiongoza ilivyotekeleza na kusimamia zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambapo kwa mara ya kwanza Tanzania imefanikisha Sensa  hiyo kidijitali.

"Kamati Kuu ya CCM pia imempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Hussein Ali Mwinyi, kwa jinsi ambavyo ameendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kiuchumi na kijamii kwa mafanikio makubwa pamoja na kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya rushwa, uhujumu uchumi na ufisadi ambavyo vinarudisha nyuma na kudumaza jitihada za maendeleo"amsema  Shaka.
Previous Post Next Post