MAGU YATAFUTA MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA WAFUGAJI KATIKA HIFADHI YA SAYAKA



Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe. Salum Kali amekutana na  viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya hiyo kujadili mikakati ya kutatua changamoto ya wafugaji katika Hifadhi ya Sayaka Wilaya ya Magu.

Kikao hicho kimefanyika leo katika  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Magu.


Mhe.Kali amesema moja ya mwarobaini wa tatizo hilo ni kujenga malambo ya kunyweshea mifugo ili kuzuia wananchi kuingiza mifugo hiyo hifadhini.


Naye, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe Mary Masanja amesema suala la uvamizi wa hifadhi ya Sayaka linatakiwa kutatuliwa kwa kushirikisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Previous Post Next Post