Na mwandishi wetu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amekabidhi eneo la mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa Miguu wa Dodoma kwa kampuni ya Limonta SPA kutoka nchini Italy ambayo itajenga uwanja huo.
Msigwa amefanya makabidhiano hayo kwa kusaini mkataba na Mwakilishi wa Kampuni hiyo Bw. Angelo Redolfi leo Jumatano, Machi 26, 2025 katika Kata ya Nzuguni jijini Dodoma, mahali ambapo uwanja huo una jengwa.
"Uwanja huu utakabidhiwa kwetu baada ya miezi 24 na Serikali itafuatilia mradi huu kwa ukaribu ili uwe wenye viwango na kukamilika kwa wakati kwa ajili ya kutumika kwenye mashindano ya AFCON 2027", amesemaMsigwa.
Serikali kupitia Wizara ilisaini Mkataba wa Ujenzi na Kampuni ya Limonta Februari 13, 2025 jijini Dodoma ambapo utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 358 na utakuwa na uwezo wa kubeba watu 32,000 pindi utakapokamilika.