ASKOFU DKT. MWAKIPESILE: MUWE TAYARI KUHESABIWA KWA MAENDELEO YETU



NA. MWANDISHI WETU

Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Dkt. Brown Abel Mwakipesile ametoa wito kwa waumini wa kanisa hilo kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na  Makazi litakalofanyika tarehe 23 Agosti, 2022 nchini.

Ametoa kauli hiyo wakati akihubiri kwenye ibada ya jumapili tarehe 21 Agosti, 2022 katika kanisa lake la EAGT Mlimwa West lililopo Maili Mbili Jijini Dodoma.


Askofu Mwakipesile alisema ni jukumu la kila muumini kuwa kielelezo kizuri katika jamii kwa kuwa tayari na kuonesha ushirikiano kwa makarani wa sensa ili kufanikisha zoezi hilo.

“Kila aliyeokoka awe mfano kwenda kuhesabiwa, popote alipo mwana EAGT ahakikishe anakuwa mstari wa mbele kushiriki zoezi la sensa,”alisema Dkt. Mwakipesile.


Aliongezea kuwa, sensa ni jambo muhimu kwa kuzingatia idadi ya watu inahitajika kila eneo ikiwemo katika kanisa ili kufanishi mipango ya maendeleo.
Previous Post Next Post