MUIGIZAJI mkongwe wa filamu nchini Mzee Korongo amefariki dunia leo Agosti 22, katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Taarifa za awali zinadai kwamba Mzee Korongo alilazwa hospitalini hapo akipatiwa matibabu siku chache kabla ya umauti kumkuta.
Taarifa za kifo hiki zimethibitishwa pia na muigizaji Monalisa kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Mzee Korongo amewahi kuigiza kwenye filamu kadhaa ikiwemo Tego, Nabii Mswahili na nyingine nyingi.
Pumzika kwa amani Mzee Korongo. Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.
………Ina Lillah Waina Ilaihi Rajuun…