KUELEKEA KILELE CHA TAMASHA LA SENSABIKA , DKT ABBAS ATOA MAELEKEZO MAZITO KWA BASATA


Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi  ametoa maelekezo mahususi kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuelekea tamasha la kihistoria la kuhamasisha Sensa kupitia Sanaa na Michezo (Sensabika).


Akizungumza na Vyombo vya Habari leo  Agosti 15, 2022 jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya kilele cha kampeni ya (sensabika) kuhamashisha sensa Agosti 21, 2022 katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam amesisitiza kuwa kuanzia sasa BASATA  wanatakuwa kutumika  kuhamasisha kila program ya Serikali kupitia Sanaa na Michezo.


Amesema Sanaa na Michezo ni nguvu laini ( soft power) ambayo ina nguvu kubwa katika kuhamasisha maendeleo ya nchi.

Amesema maadhimisho ya kilele cha tamasha hilo la kistoria yamekamilika na ametoa wito kwa wananchi note nchini kuhudhuria.





Ameongeza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na michezo mbalimbali na sanaa mbalimbali za maonesho ikiwa ni pamoja na jogging.

Amesema mbali na  ni  michezo ya hapa nyumbani  pia mchezo wa yoga utachezwa kwa kuongozwa na kampuni ya Arts of Living.

Katika hatua nyingine Dkt. Abbasi ametumia  jukwaa hilo kuelezea mafanikio makubwa yaliyojitokeza  kutokana na Royal Tour.

Ameyataja mafanikio ya ujumla kuwa Royal tour imefungua milango ya kila sekta duniani.
Katika mkutano huo Dkt. Abbasi aliambatana na  viongozi wakuu wa mashirikisho na mabaraza ya michezo ambao walipata fursa ya kuchangia kwa ufupi ushiriki wa wadau wao kwenye tamasha

Previous Post Next Post