SHIRIKA LA NDEGE (ATCL) YAFANYA ZIARA KWENYE KAMPUNI YA SKYLINK ,UPANUAJI WA MTANDAO SAFARI.



Na Lilian Ekonga

SHIRIKA la Ndege nchini(ATCL),limesema litaendelea kuboresha huduma mbambali za shirika hilo ikiwemo kuongeza safari nyingi za nje ya nchi ili kuweza kuendana na soko la kimataifa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi ATCL,Mhandisi Ladislaus Matindi,wakati alipokuwa akuwa akitembelea kampuni  ya  uwakala wa ticketi za ndege ya  Skylink Travel and Tours iliyopo jijini hapa 

Matindi amesema baada ya kufanya vizuri kwenye soko la nchi ya Jamhuri ya Kongo kwa sasa wanajiandaa kwenda nchi za Afrika magharibi hapo mwakani baada ya ujio wa ndege tano hivyo jambo lilopo sasa kwa ATCL ni kutatua changamoto  zinazoikabili.

Aidha,Matindi amesema kwa sasa wamebaini kuna changamoto kwenye suala la tiketi ikiwemo Abiria kuchelewa kupata tiketi zinazochongiwa na kusuasua kwa baadhi ya kampuni za ukataji tiketi na kuwataka makampuni hayo kutatua changamoto hiyo kwa kuwataka wateja kuweka umakini katika ukataji tiketi.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya  Skylink Travel and Tours,Moustafa Khataw , amesema kampuni hiyo itaendelea kuboresha huduma zake ili ziweze kuendana na hadhi ya ATCL.
Previous Post Next Post