Na Lilian Ekonga
Makumbusho ya Taifa la Tanzania Kwa kushirikiana na wadau mbali mbali inaandaa mbio za hiari zijulikanazo kama Mwl. Nyerere Marathon zenye lengo la kukusanya kiasi Cha 300, 000,000 ikiwa ni sehemu ya Programu ya Miaka 10 ya kuenzi na kutangaza Urithi wa Mwl. Julius Kambararage Nyerere, Muasisi wa Taifa la Tanzania zinazo tarajiwa kufanyika tarehe 01 oktoba 2022.
Akizungumza na Waandishi Habari Mkurugenzi MKuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Noel Lwoga amesema mbio za hiari za Mwl. Nyerere ni sehemu ya mpango wa miaka 10 ya kuenzi na kutangaza Urithi wa Mwl Nyerere uliozinduliwa na Waziri MKuu Mstaafu Mhe. Peter Kayanza Mizengo Pinda Tarehe 13 April 2022 Butiama.
Amesema Mbio hizi zinalenga kuanzisha zao jipya la utalii kupitia michezo za kukusanya michango ya fedhaza hiari Kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya makumbusho na vituo vya malikale vya kumbukizi ya Mwl Nyerere ambao unaratibiwa na Makumbusho ya Taifa.
"Mbio hizi ni za kipekee Kwa Sababu zinahusisha Siku, mwezi na mwaka alizaliws Mwl. Nyerere yaani Tarehe 13 April 1992, hivyo kitakuwa na mbio za kilomita 22 zenye washiriki 300, mbio za kilomita 13 zenye washiriki 300, mbio za kilomita 4 zenye washiriki 200 amabo ni viongozi na watumishi mbali mbali na washiriki wengine 200 ambao ni wanafunzi wa shuleza msingizi na sekondari" amesema Noel Lwoga.
Pia amesema njia itakayotumika Katika mbio hizo ni Barabara ya Butiama kwenda Busegwr Kwa Sababu imebeba historian Kwa Maana ndiyo aliyoitumia mwlm Nyerere kwenda shuleni wakati anasoma shule ya Msingi Mwisengi.
Aidha amesema gharama za ushiriki WA mbio hizo ni sh Elfu Thelathini (30,000) Kwa watu wazima na Tzs 5000 Kwa wanafunzi na wanatarajia kuwa na washiriki zaidi 1000 Kwa mbio zote
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya mwalimu Nyerere amesema maandalizi yapo vizuri na Kwa uapnde wa baskeli Kuna wadau ambao wao walishirikia Katika miaka 100 ya mwalimu Nyerere na tumeshawasiliana nao na watashiriki pamo