Na Humphrey Msechu, Mbeya
KAIMU mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Primus Kimaryo Amesema kuwa maonyesho ya kitaifa ya 88 ambayo yamefanyika jijini Mbeya yamekuwa na mwitikio mkubwa sana na wao kama bodi ya kahawa wameweza kuonyesha mnyororo mzima wa thamani kuanzia kwenye kulima,matumizi ya mbolea kwa kushirkiana na wenye viwanda na wakaangaji na kuonyesha bidhaa zao kwenye maonyesho hayo.
Amesema kuwa kupitia maonyesho hayo wameweza kutoa huduma kuanzia utoaji wa leseni mbalimbali pamoja na vibali kuonyesha masoko yanavyokwenda hivyo kwa maana hiyo huduma zote wameweza kuzipata kwenye banda hilo.
kimaryo ameyasema hayo mkoani mbeya Agosti nane katika kilele cha maonyesho 88 ambapo amefafanua kuwa kahawa ni moja ya zao la kimkakati na mkakati uliopo ni kwamba serikali imewaelekeza ifikapo mwaka 2025/26 wawe wamezalisha tani laki tatu na mkakati waliojiwekeza ni katika maeneo makubwa matatu ambayo ni kuongeza tija ya uzalishaji.
Mkakati mwingine ni kuongeza bei ya mkulima pamoja na kuweka mazingira mazuri ya biashara hivyo kwenye kuongeza tija ya uzalishaji bodi ya kahawa imepanga kuzalisha miche milioni 20 kwa miaka mitano ijayo ma wanafanya hivyo na mwitikio ni mkubwa sana wa miche lakini kama alivyosema waziri wa kilimo Hussein Bashe kuhusu suala zima la mbolea ,Pembejeo pia imewekwa ndani ya sekta hiyo na wakulima watakuwa wanapata kwa shilingi elfu 70.
"Hii inamaana kubwa kwamba sambamba na hili kwenye bei ya mkulima kuongeza wanunuzi na kupata soko la moja kwa moja ili mkulima aweze kupata bei na tunasaidiana na vyama vya ushirika ili kuweza kuuza nje ya nchi moja kwa moja katika masoko maalum "Amesema
Ukija kwenye soko zima la mazingira ya biashara serikali imepunguza tozo nyingi sana kwenye sekta ndogo ya kahawa na kuhakikisha anapata kipato kikubwa ikilinganishwa na huko nyuma hivi sasa tunahakikisha kunakuwa kuna sera zinazokidhi kwa miaka mingi ijayo na kunakuwa na uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo cha kahawa".
Kimaryo Amesema kuwa eneo kubwa ambalo wanaona ni changamoto ni kuuza kahawa nje ya nchi kwani janga la korona limetoa funzo kwani unapotegemea soko la nje ya nchi na kunapotokea majanga kama korona ni changamoto kwa wakulima wetu hivyo ni kuhakikisha kuna kuwa na uwekezaji katika viwanda vya ndani na unywaji wa kahawa nchini.
"Kimsingi unywaji wa kahawa bado ni mdogo ni asilimia tano mpaka saba hivyo tunahitaji kuweka mkakati mpana wa kuwekeza kwenye kahawa pamoja na kuhusuka kwenye unywaji wa kahawa ndio itakuwa suluhisho la kuongeza soko la ndani."amesema
Ameongeza kuwa zao la kahawa bado linalipa sana kama kauli mbiu iliyopo sasa kwamba kilimo ni biashara wito ni kuhakikisha uwanalima kwa tija kwa wakulima ni kulima kwa kiwango kinachotakiwa na kutoka kwenye taasisi ya utafiti ni kwamba mkulima anapokuwa na miti 540 anapata faida kwa hali ilivyo sasa bei ni mzuri wakulima wanapata faida.
Amesema wakulima wawekeze kwenye kilimo cha kahawa ni mali lakini si tu kuwekeza pia wawekeze kwenye viwanda vya kahawa na maduka ya kahawa lakini pia kujihusisha zaidi kwenye unywaji wa kahawa ,kahawa ni bora hata kwa afya.