DC JOKETI AZINDUA TAWI LA BENKI YA TCB, MBAGALA



Mkuu wa wilaya ya Temeke Joketi mwegelo amezidua tawi jipya la Benki ya Tanzania commercial Bank(TCB) katika eneo la Mbagala katika mwendelezo wa kuwainua kuichumi  wakazi wa mbagala kupitia mikopo inayotolewa na TCB Banki.

Akizungumza na  wakazi wa mbagala wakati  Uzinduzi wa Tawi Hilo   DC Joketi amesema Benki ya biashara Tanzania inatoa huduma mbalimbali za kifedha ikiwa ni pamoja na Utunzaji wa fedha, Akaunti za watoto, vikundi, wavuvi, Mikopo mbalimbali ya wakulima,wastaafu wafanyabiashara, watumishi wa Umma, mikopo na nyumba.



"Dirisha maalum la wanawake lenye akaunti mahususi kwa wanawake inayoitwa Tabasamu ambalo mnamomwaka 2021 Benki, ilifanikiwa kuandaa makongamano kwenye mikoa mbalimbali kwa ajili ya kujadili maswala mbalimbali ikiwemo nafasi ya mwanamke katika kukuza uchumi".amesema DC Joketi

Aidha amessma Ujio wa tawi la mbagala ni hatua muhimu sana katika utekelezaji wa mikakati yetu ya kukuza uchumi , tunamatumaini kuwa benki itatatua changamoto za wananchi wa mbagala na itaendelea kutoa elimu na fursa mbalimbali zinazotolewa na benki kwa wakazi wa Mbagala. 

Pia ametoa  wito kwa benki kutoa huduma za mikopo nafuu ili kuwafikia wafanyabiashara, wakina mama na jamii nzima katika kuendelea kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Benki ya TCB, Moses Manyata amesem katika mkoa wa Dar Es Salaam Benki ya Biashara Tanzania ina jumla ya
matawi 20 hivyo basi wananachi wa Mbagala mnakaribishwa katika kufungua akaunti ili
kihifadhi fedha na pia kupata mikopo mbalimbali ili waweze  kuinuka kiuchumi.



Amesema  Tawi la Mbagala lina jumla ya wateja
47,748 wanaofurahia huduma mbalimbali za kibenki hususani mikopo yenye riba nafuu
kama ya kilimo, biashara, watumishi na wastaafu pamoja na kufanya miamala mbalimbali ya
kifedha ndani na nje ya nchi. 

"Kwa kipindi cha mwaka 2021 mpaka 2022 tawi limefanikiwa kufikia mikopo yenye thamani ya Bil 7.2 kwa jumla ya wateja 564 ni matarajio  yetu kuwa biashara itaendelea kukua na kutuwezesha kufunga matawi" Amesema



Previous Post Next Post