MKUU WA WILAYA YA KALAMBO MHE. TANO MWERA AZINDUA RASMI USAJILI WA MBOLEA ZA RUZUKU KWA WAKULIMA



Mkuu wa Wilaya ya Kalambo iliyopo Mkoani Rukwa Mhe Tano Mwera akiwa katika picha ya pamoja wakati wa kikao hicho cha Kamati ya mazao cha Wilaya

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo iliyopo Mkoani Rukwa Mhe Tano Mwera akiongoza kikao cha Kamati ya mazao cha Wilaya


Na Mwandishi Wetu, Kalambo.

MKUU wa Wilaya ya Kalambo, iliyopo Mkoani Rukwa, Mhe. Tano Mwera amezindua rasmi usajili wa mbolea za ruzuku huku akiwataka Wakulima kutoa taarifa sahihi na kuepuka udanganyifu kwa Serikali.

Mhe. Tano Mwera amefanya uzinduzi huo wakati wa kikao cha Kamati ya mazao cha Wilaya hiyo ya Kalambo, kilichowakutanisha wadau mbali mbali,

Ambapo amesema kuwa, kila Mkulima anayetaka Mbolea ajisajili kwa Mtendaji wa Kijiji ambapo shamba lake lipo sambamba na kuwa na nyaraka muhimu zinazomtambulisha Kisheria.


"Katika Usajili Mkulima, atahitajika kuwa na Kitambulisho cha NIDA au cha Mpiga kura ama hati ya kusafiria au leseni ya udereva.

Lakini pia atataja eneo la ukubwa wa Shamba lake na mazao anayolima." Alibainisha Mkuu wa Wilaya Mhe Tano Mwera.

Ambapo amesisitiza kwa Wakulima kutoa taarifa sahihi na kuepuka udanganyifu ili Serikali iweze kuleta Mbolea sahihi kwa wakati sahihi kutokana na mahitaji.

Serikali katika Mwaka wa Fedha wa 2022/2023, imetenga kiasi cha shilingi bilioni 150 kugharamia ruzuku ya mbolea itakayo tolewa kwa Wakulima wote Nchini. 

Ambapo kengo ni kutoa Ruzuku ili kupunguza makali ya bei ya Mbolea kwa Wakulima ili kuongeza Mchango wa sekta ya Kilimo katika pato la taifa

Previous Post Next Post